Teknolojia mpya ya barabara zinazochaji magari

0
306

Ujerumani imeanza kuwekeza katika mradi wa teknolojia mpya ya ujenzi wa barabara zenye uwezo wa kuchaji magari bila ya kutumia waya, hii itakuwa ni teknolojia mpya zaidi kwa nchi zilizoendelea.

Mradi huo unatekelezwa na kampuni bobevu ambayo ndio msambazaji mkuu wa magari hayo ya umeme yanayochaji bila ya kutumia waya yatakayotumika kutoa usafiri wakijamii na wakibiashara.

Teknolojia hii inafanya kazi kwa kuchaji gari pale linapokuwa katika mwendo au likiwa limesimama katika barabara maalumu.

Mpango huu unakuja baada ya majaribio ya mafanikio ya teknolojia ya Electreon huko Karlsruhe, moja ya miji mikuu ya Ujerumani ambapo ilijengwa barabara ya umeme katika kituo cha mafunzo cha EnBW.

Ili kukamilika kwa mradi huo inategemewa kutumika zaidi ya dola zakimarekani milioni 3.4 kusimika miundombinu hiyo katika barabara za mijini.