SMS kongwe zaidi yafikisha miaka 30

0
314

Hivi ndivyo ulivyosomeka ujumbe wa kwanza wa simu ya mkononi uliotumwa miaka 30 iliyopita mnamo Desemba 1992.

Mhandisi wa kampuni ya Vodafone Neil Papworth kwa kipindi hicho alikuwa akijaribu teknolojia  mpya kwa kutuma ujumbe wa maandishi kwa mmoja wa viongozi wakubwa wa mtandao huo wa simu ambaye alikuwa kwenye sherehe ya Krismasi.

Hata hivyo ujumbe wake haukujibiwa.

Hadi sasa ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) bado unatumika ambapo hadi sasa SMS bilioni 40 zimetumwa nchini Uingereza kwa mwaka 2021.

Hata hivyo idadi hiyo ya SMS inatajwa kuwa ni ndogo kulinganisha na zile za jumbe za whatsapp ambazo jumbe bilioni 100 hutumwa duniani kote kila siku.

Ujumbe huo wa kwanza wa maandishi uliingizwa sokoni na kuuzwa kama NFT mwaka 2021.