UJUMBE WA MISA YA MKESHA WA KRISMASI

0
202

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, Isaac Amani amewasihi waumini wa dini ya kikrito kuzingatia mambo haya ili kusherekea Krismasi kwa imani kadri ya mafundisho ya neno la Mungu.

Kulea watoto vizuri
“Tuwafundishe kujitegemea na malezi yawe ya kujenga tabia nzuri katika kristo.”

Tunapaswa kuwa na shukurani
“Si kula na kuvaa bali kuishi lengo la Krismasi kushukuru na kusaidia pia.”

Tuwe na hekima na utii
“Kama Yesu aliyeonesha kwa matendo yake na sisi tuwe wanafunzi bora kwa matendo.”

Tushirikiane kuanzia ngazi ya familia
“Utandawazi usiteke mahusiano katika familia au jamii bali uwepo wa Mungu uonekane.”

Tuoneshe imani kwa matendo
“Uwepo wa matunda yakutendeana haki, ukarimu hata katika magumu ya maisha tusimamie upendo na haki.”

Kuomba baraka
“Kuombea nchi baraka hasa kwenye mazingira magumu yote ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi, Mungu aliumba misitu na sisi kwa kukata miti tunajenga majangwa tunahitaji kubadilika.”

Askofu Isaac Amani ameyasema hayo wakati akiongozwa Misa ya Mkesha wa Krismasi Kitaifa katika Kanisa Kuu Katoliki la Mt. Theresia wa Mtoto Yesu jijini Arusha.