Mapokezi ya Morocco

0
253

Timu ya Taifa ya Morocco imepokelewa kwa shangwe kubwa baada ya kumaliza katika nafasi ya nne kwenye mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.

Morocco imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kufika hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo makubwa zaidi duniani.

Baada ya kurejea, wachezaji na benchi la ufundi walipokelewa na Mfalme Mohammed VI na kuvishwa nishani ya kifalme.