Kapembe wa TBC kuzikwa leo

0
116

Mazishi ya mpiga picha na mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Joachim Kapembe, yanafanyika leo alasiri katika makaburi ya Kange mkoani Tanga.

Shughuli za mazishi zinaendelea hivi sasa mkoani Tanga, ambapo itakapofika saa sita mchana itafanyika Ibada ya mazishi.

Joachim Kapembe ambaye kituo chake cha kazi kilikuwa mkoani Manyara, alifariki dunia tarehe 13 mwezi huu baada ya kupata ajali ya baiskeli akishuka kutoka kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro.

Ameacha mke na watoto wawili.