UVCCM watakiwa kufanya siasa kistaarabu

0
121

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, amewataka wanachama wa Umoja wa Vijana wa chama hicho ( UVCCM) kufanya siasa za kistaarabu na kubishana kwa hoja.

Dkt. Mwinyi ambaye pia ni Rais wa Zanzibar ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa UVCCM Taifa chini ya Mwenyekiti wake mpya Mohammaed Kawaida.

Pia amewataka kuendelea kuhubiri amani kwa kuwa ndio tunu kwa Taifa lolote lile duniani.

Dkt. Mwinyi amewaeleza viongozi hao wa UVCCM kuwa vijana wana nguvu kubwa katika jamii, hivyo atashirikiana nao katika masuala mbalimbali ya chama na ya kuiimarisha jamii.

Kwa upande wake Mwenyekiti huyo wa Umoja wa vijana wa CCM Mohammed Kawaida ameahidi kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mambo mbalimbali inayoyatekeleza.