Kiwanda cha maziwa chazinduliwa Nsimbo

0
103

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua kiwanda cha kuchakata maziwa cha MSS kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi, ambacho kina uwezo wa kusindika wastani wa lita elfu 10 za maziwa kwa saa.

Akizungumza baada ya kuzindua kiwanda hicho ambacho uwekezaji wake umegharimu shilingi milioni 600, Waziri Mkuu Majaliwa amesema, Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji
ili kila mwenye uwezo awekeze.

Kiwanda hicho cha kuchakata maziwa cha MSS kwa sasa kinazalisha maziwa ya mtindi na maziwa fresh na kinatarajiwa kuanza uzalishaji wa samli hivi karibuni.

Waziri Mkuu ametoa rai kwa wafugaji wanaozunguka kiwanda hicho kuuza maziwa yao kwa mwekezaji huyo ili waweze kujiongezea kipato na kumwezesha mwekezaji huyo kuwa na uhakika wa malighafi ya kutosha.