Kampuni kubwa ya vifaa vya teknolojia ya Huawei ya nchini China imeishitaki serikali ya Marekani kwa kuathiri biashara ya kampuni hiyo baada ya kuzuia bidhaa zake kuuzwa Marekani kwa madai kuwa imekiuka vikwazo vya biashara.
Mgogoro kati ya kampuni hiyo na Marekani ulianza baada ya nchi hiyo kuamuru mmoja kati ya viongozi wa kampuni hiyo na muasisi wa Huawei, kutiwa mbaroni na kupelekwa nchini Marekani, akiwa nchini Canada ili ashitakiwe.
Marekani ilidai kuwa kampuni hiyo imekiuka vikwazo ambavyo nchi hiyo ilikuwa imeiwekea Iran, na badala yake Huawei imekuwa ikiuza bidhaa zake nchini Iran kinyume cha vikwazo vipya dhidi ya nchi hiyo.
Huawei imekunusha tuhuma hizo na kusema kuwa kampuni hiyo imekuwa na mawasiliano ya karibu na maafisa usalama wa Marekani, hivyo haiwezi kufanya makosa kama hayo, kwani kila jambo la kibiashara lenye utata kampuni hiyo imekuwa ikiwauliza maafisa hao.