Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela, – Juan Guaido ameitisha maandamano ya nchi nzima siku ya Jumamosi Machi Tisa mwaka huu, kupinga utawala wa Rais Nicolas Maduro.
Guaido ambaye pia amejitangaza Rais wa Mpito wa Venezuela ameyasema hayo mara baada ya kurejea nchini humo akitokea katika ziara yake ya nchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Brazil, Argentina, Colombia, Ecuador na Paraguay ambapo alikwenda kwa lengo la kutafuta kuungwa mkono.
Akihutumia mamia ya Raia wa Venezuela waliojitokeza kumlaki katika mji mkuu wa Venezuela, – Caracas, Guaido amesema kuwa maandamano yataendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na hawatapumzika mpaka kile alichodai uhuru kipatikane.
Guaido amerejea nchini Venezuela licha ya hofu ya kukamatwa, kwa madai ya kukiuka amri ya kutosafiri aliyopewa na mamlaka za nchi hiyo.