Ugonjwa wa Kimeta wadhibitiwa

0
571

Katibu Mkuu wa wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Profesa Elisante Ole Gabriel amesema kuwa ugonjwa wa Kimeta umedhibitiwa na hivi sasa wizara inaendelea kutoa elimu kwa wafugaji kuhusu namna ya kujikinga na ugonjwa huo.

Profesa Ole Gabriel ametoa kauli alipofanya ziara katika mnada wa Pugu uliopo jijini Dar es salaam kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali katika mnada huo.

Katibu Mkuu huyo wa wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo amelazimika kutoa kauli hiyo kufuatia baadhi ya Watanzania hasa walaji wa nyama kuwa na wasiwasi kuhusu uwepo wa ugonjwa huo wa Kimeta.

Amesisitiza kuwa serikali kupitia wizara ya Mifugo na Uvuvi. imekwishapeleka chanjo kwa wafugaji katika maeneo mbalimbali nchini ili kudhibiti ugonjwa huo hatari.