Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria amerejesha fomu yake ya kugombea urais katika ofisi za Tume ya Uchaguzi nchini Algeria mjini Algiers, licha ya kufanyika kwa maandamano makubwa yenye lengo la kupinga hatua hiyo.
Mamia ya Raia wa Algeria siku ya Jumapili walijitokeza katika mitaa mbalimbali ya nchi hiyo kupinga hatua ya Bouteflika kutaka kugombea tena urais kwa muhula wa tano, huku afya yake ikiwa imedorora.
Raia hao waliingia katika siku ya kumi ya maandamano yao siku ya Jumapili ambayo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kwa wagombea wa kiti cha urais kurejesha fomu zao za maombi ya kugombea kiti hicho cha Urais katika Tume ya Uchaguzi.
Bouteflika ambaye alipata kiharusi tangu mwaka 2013, na tangu wakati huo amekuwa akitibiwa nchini Morocco, amesema kuwa bado ana uwezo wa kuiongoza Algeria.
Bouteflika ana umri wa miaka 82.