Serikali kuendelea kuhudumia Wananchi

0
93

Serikali imesema itaendelea kuzingatia maelekezo Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati na maeneo yote yaliayoainishwa katika ilani ya chama hicho pamoja na kuimarisha huduma kwa wananchi .

Akizungumza mkoani Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya serikali ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika miradi ya maendeleo wakati wa mkutano mkuu wa 10 wa CCM, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali itaendelea kufanyia kazi maeneo yote yenye changamoto.

Aidha, amesema serikali itaendelea kupokea maelekezo ili kuimarisha utendaji kazi ndani ya serikali, utendaji wenye uadilifu na uaminifu.