Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapiduzi ya Zanzibar kwa utekelezaji wa ilani ya CCM kwa vitendo.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za CCM kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita wakati wa siku ya pili ya mkutano mkuu wa 10 wa Chama Cha Mapinduzi unaofanyika mkoani Dodoma, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Christina Mndeme amesema chama hicho kimeridhika na utekelezaji wa ilani yake baada viongozi mbalimbali kupita katika maeneo yote nchini kukagua utekelezaji wa ilani unaofanywa na serikali zote mbili.
Mmdeme ameongeza kuwa, malengo ya CCM na Jumuiya zake kwa mwaka 2022 hadi mwaka 2027 ni kusimamia utendaji kazi wa viongozi na maadili ya wanachama, pamoja na kuzisimamia serikali zote mbili katika kutekeleza sera za CCM na Ilani ya uchaguzi .