Wajumbe wa mkutano mkuu wa kumi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), viongozi mbalimbali pamoja na wageni waalikwa wa mkutano huo wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma ikiwa ni siku ya pili na ya mwisho ya mkutano huo.
Ajenda mbalimbali zinawasilishwa katika siku hiyo ya pili ikiwa ni pamoja taarifa ya Halmashauri Kuu ya CCM ya utekelezaji wa kazi za chama na Jumuiya zake kwa kipindi ha miaka mitano (2017 – 2022).
Ajenda nyingine ni taarifa za serikali ya Jamhurri ya Muungano wa Tanzania na ile ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi katika kipindi cha mwaka 2020 – 2025.