Mbungi la Robo Fainali ya Kombe la Dunia ipo pale pale! Mechi zenye msisimko wa aina yake ndio zinaanza.
Ijumaa hii robo fainali ya 1998 inajirudia kwa Argentina kuwakabili Uholanzi katika mechi wanayohitaji kulipa kisasi kupoteza mchezo huo kwa bao 2-1.
Vijana wa Mwalimu Lionel Scaloni wanawaza namna ya kuvuka hatua hii na matumaini yao makubwa ni kuwania Ubingwa wa michuano hii kwa mara ya mwisho ya nyota wao Lionel Messi kama mchezaji.
Luis Van Gaal na kijana wake wa dhahabu msimu huu Coady Gakpo bado wanataka kuendeleza kile walichokifanya miaka 24 iliyopita. Wapo kwenye kiwango kizuri pia mpaka sasa.
Usikose kufuatilia mechi hizi mbashara kupitia TBC.