Bunge SA lasitisha uamuzi kumhusu Ramaphosa

0
328

Baada ya Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini kukumbwa na kashfa za rushwa, bunge la nchi hiyo lilipanga kupiga kura hii leo kuamua kama Rais huyo afunguliwe mashtaka na kuondolewa madarakani, suala ambalo limesitishwa kwa muda.

Mapema hii leo chama tawala cha nchini Afrika Kusini cha African National Congress (ANC) kilisema, kiko pamoja na Rais Ramaphosa na kuwa wabunge wake watapiga kura kupinga kuondolewa madarakani.

“Awali kura hiyo ilipangwa kufanyika Jumanne, lakini sote tumekubaliana Desemba 13.” amesema mmoja wa wabunge hao Nosiviwe Mapisa-Nqakula

Kesi ya Rais Ramaphosa ilianza mwezi Juni mwaka huu wakati mkuu wa zamani wa ujasusi wa nchi hiyo Arthur Fraser kuwasilisha malalamiko kwa polisi akidai Rais Ramaphosa alificha wizi uliotokea mwezi Februari mwaka 2020.

Rais Ramaphosa pia anadaiwa kuficha dola milioni nne za kimarekani kwenye sofa nyumbani kwako, jambo ambalo halikuwahi kufahamika.