Rais Donald Trump wa Marekani amesema kuwa hatotangaza viwango vipya ya ushuru kwa bidhaa za China zenye thamani ya Dola Bilioni 200 za Kimarekani.
Marekani ilitarajiwa kuongeza ushuru kwenye bidhaa zinazotoka China kutoka asilimia 10 hadi 25 kuanzia Machi Mosi mwaka huu.
Uamuzi huo wa Rais Trump huenda ukaondoa hofu kuwa vita vya kibiashara kati ya Marekani na China, nchi ambazo ni kubwa kiuchumi duniani vitakuwa vikali zaidi katika muda mfupi ujao.
Trump amefikia uamuzi huo katika kipindi hiki ambapo wajumbe kutoka Marekani na China wakiendelea na mazungumzo yao ya siku sita mjini Washington, mazungumzo yenye lengo la kujadili masuala ya kibiashara.