Simba wakiwa na kigugumizi kiasi kimatokeo wanazisaka alama 3 muhimu kwa Askari Polisi wa Tanzania pale Moshi kwenye uwanja wa Ushirika! Polisi pia ana wakati usioridhisha kwenye Ligi msimu huu lakini wanarejea nyumbani baada ya kuwa Arusha kwa muda.
Polisi wameshinda mchezo mmoja tu kati ya mitano iliyopita na Simba wameshinda mitatu na sare 2 kwenye Ligi Kuu NBC.
Historia bado inamkaba Polisi kwani amefungwa michezo 5 dhidi ya Simba na mara Moja tu akipata sare katika makutano ya wao kwa wao!.
Azam FC wapo kwenye mwendo mzuri sana wanawakaribisha wana Mangushi, Coastal Union kutoka Tanga pale Chamazi.
Tangu 2018 Azam kashinda mechi 2 dhidi ya Coastal, kafungwa 2 na sare 4 zimeshuhudiwa baina yao!
Hizi ni mechi kali kabisa za Ligi Kuu NBC Tanzania Bara ambazo utazisikiliza kupitia TBC FM na TBC Online mbashara kuanzia saa 10:00 jioni na saa 1:00 usiku pale Chamazi.