Rais Weah asherehekea goli la mwanaye

0
1827

Rais George Weah wa Liberia pamoja na mkewe wamepata chakula cha jioni na mtoto wao Timothy Weah (22) kama sehemu ya kusherehekea goli la Timothy aliloifungia Marekani dakika ya 36 dhidi ya Wales katika mchezo wa sare ya 1-1 wa Kombe la FIFA la Dunia nchini Qatar.

Timothy amechagua kuwa raia wa Marekani kutokana na kuzaliwa New York mwaka 2000 ila mama yake ana asili ya Jamaica na Baba yake ndio Rais wa Liberia kwa sasa.

Weah ambaye ni Rais wa Liberia tangu mwaka 2018, ndio mchezaji pekee wa Afrika kuwahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia (Ballon d’Or) mwaka 1995, lakini hajawahi kucheza fainali zozote za Kombe la Dunia