Saudi Arabia yatangaza mapumziko kwa kuifunga Argentina

0
226

Baada ya ushindi wa kihistoria dhidi ya Argentina, Mfalme Salman wa Saudi Arabia ametangaza Jumatano, Novemba 23, 2022 kuwa siku ya mapumziko.

Likizo hiyo inawahusu watumishi wa sekta ya umma na sekta binafsi pamoja na wanafunzi kwenye ufalme huo, ili kushangilia ushindi huo.

Tukio hilo ni sawa na lililotokea mwaka 1990 ambapo Cameroon ilitangaza mapumziko kwa Taifa zima baada ya kufinga Argentina kwenye Kombe la Dunia nchini Italia.

Kabla ya mchezo wa leo, Saudi Arabia ilikuwa imeshinda michezo mitatu tu katika historia yake ya kushiriki mashindano hayo makubwa duniani.

Jumamosi Saudi Arabia itavaana na Poland, kisha Jumanne watakamilisha michezo ya makundi kwa kuikabili Mexico.