Venezuela yavunja uhusiano wa Kidiplomasia na Colombia

0
680

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela ametangaza kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Colombia.

Taarifa iliyotolewa na serikali ya Venezuela imesema kuwa Maduro pia amewaamuru wawakilishi wa Kidiplomasia wa Colombia waliopo Venezuela kuondoka ndani ya muda wa saa 24.

Rais Maduro amechukua uamuzi huo kwa madai kuwa Colombia imekua ikitoa msaada kwa kiongozi wa upinzani Juan Guaido , aliyejitangaza kuwa ni Rais wa mpito wa Venezuela.

Tayari rais Maduro amezuia misaada ya kibinadamu kuingizwa nchini Venezuela kutoka katika nchi za Brazil na Colombia.

Malori 14 yaliyokuwa na tani 280 za chakula na dawa yamezuiliwa katika mpaka wa Venezuela na nchi hizo, na hivyo kufanya maisha ya raia wengi wa nchi hiyo kuendelea kuwa mashakani.

Hatua hiyo ya kuzuiliwa kwa misaada ya kibinadamu nchini Venezuela imezusha ghasia zilizosababisha vifo vya watu kadhaa na kuchomwa moto kwa baadhi ya malori yaliyobeba msaada huo.