Majeruhi waendelea na matibabu

0
688

Majeruhi Wanne wa ajali ya gari iliyotokea wilayani Kilombero mkoani Morogoro na kusababisha vifo vya watu wengine Tisa, wanaendelea kupatiwa matibabu.

Ajali hiyo imetokea Jumamosi Februari 23 baada ya gari aina ya Land Cruizer iliyobeba Wafanyakazi 13 wa Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi (LTSP) kutumbukia katika mto Kikwawila.

Habari zaidi kutoka mkoani Morogoro zinaeleza kuwa, dereva wa gari hilo alishindwa kulimudu, na hivyo kutumbukia mtoni.

Mkuu wa wilaya ya Kilombero, – James Ihunyo amesema kuwa majeruhi wa ajali hiyo wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Mtakatifu Francis iliyopo Ifakara.

Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi iko chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.