Yanga yaisambaratisha Singida Big Stars

0
170

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka ya NBC, Yanga SC wamerejea kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo baada ya kuipa kichapo cha mabao 4-1 walima alizeti wa Singida Big Stars.

Fiston Mayele amerejea kwenye ubao wa magoli baada ya kufunga ‘Hat-trick’ katika mchezo huo ambao Yanga wameutawala kwa dakika zote 90.

Mayele amefunga katika dakika ya 16, 27 na 56 huku Kibwana Shomari akifunga katika dakika ya 48.

Bao la kufutia machozi kwa Singida Big Stars limefungwa na Meddie Kagere katika dakika ya 66 ya mchezo huo.

Huu unakua ushindi wa kwanza mkubwa kwa Yanga tangu kuanza msimu huu wa Ligi kuu ya soka ya NBC.