Picha za Ronaldo zaondolewa Old Trafford

0
216

Maafisa wa uwanja wa Old Trafford wameanza kuondoa mabango yenye picha za nyota wa klabu hiyo na timu ya Taifa ya Ureno Christiano Ronaldo.

Picha mbalimbali zimewaonesha maafisa wa uwanja huo wakibandua picha hizo ambazo zimewekwa kuzunguka uwanja wa Old Trafford.

Mapema wiki hii jina la Ronaldo liligonga vichwa vya habari katika maeneo mbalimbali duniani baada ya nyota huyo wa soka kueleza mambo kadhaa yanayozunguka klabu ya Manchester United katika mahojiano ya “Talk Tv” yaliyoendeshwa na Piers Morgan.