Same na Mwanga wapata majengo mapya ya mahakama

0
142

Majengo mapya ya mahahama za wilaya za Mwanga na Same mkoani Kilimanjaro, yamezinduliwa rasmi hii leo na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma.

Ujenzi wa majengo ya mahakama hizo ulianza mwezi Februari mwaka 2021 na umekamilika mwezi Agosti mwaka huu.

Shilingi milioni 726.9 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa jengo la mahakama ya wilaya ya Mwanga na shilingi milioni
724.9 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa jengo la mahakama ya wilaya ya Same.

Fedha za ujenzi wa majengo hayo ya mahakama zimetokana na fedha za ndani, ikiwa ni mpango wa mahakama wa kuendelea kuboresha miundombinu yake pamoja na kusogeza karibu huduma ya utoaji haki kwa wananchi.