Wapenzi, Kitimoto, Pombe marufuku Qatar

0
257

Wenyeji wa kombe la FIFA la Dunia mwaka huu nchi ya Qatar imeendelea na msimamo wake wa kukata kuingizwa bidhaa kama sex toys, matumizi ya pombe isipokuwa kwa mpangilio maalum, wamezuia pia nyama ya nguruwe na endapo utabeba vyote vitabaki uwanja wa ndege na kwenye vizuizi na havitorudishwa kwa muhusika.

Licha ya kupiga marufuku mapenzi ya jinsia moja, pia wamezuia watu ambao sio wanandoa kufanya mapenzi na endapo utabainika utakumbana na kifungo cha miaka saba jela.