Mradi wa maji Kigamboni wazinduliwa

0
162

Rais Samia Suluhu Hassan, leo amezindua mradi wa maji Kigamboni, katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Kisarawe II – Kigamboni mkoani Dar es Salaam.

Mradi huo wa maji una uwezo wa kuzalisha takribani lita milioni 70 za maji safi kwa siku kwa ajili ya kuhudumia wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Kwa wilaya ya Kigamboni pekee zitatumika lita milioni 25 za maji huku lita 45 zilizobaki zitasambazwa katika wilaya nyingine za mkoa wa Dar es Salaam na lita nyingine zitasambazwa mkoani Pwani.