Yanga kutua nchini leo

0
219

Baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, Mabingwa wa Tanzania Yanga wanatarajiwa kuwasili nchini mchana wa leo.

Yanga wameondoka nchini Tunisia jana jioni kurejea Tanzania wakipitia Dubai, Falme za Kiarabu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika Klabu hiyo, Yanga itasafiri tena majira ya saa 3 usiku kwenda Jijini Mwanza ambapo Jumapili watakuwa wageni wa Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi kuu ya soka ya NBC.

Yanga wanarejea nyumbani wakiwa na heshima ya ushindi wa bao moja kwa sifuri iliyoupata mbele ya Club Africain ya Tunisia.