Marekani ya kwanza kuwasili Qatar

0
221

Timu ya Taifa ya Marekani imekuwa timu ya kwanza kuwasili nchini Qatar kati ya timu za mataifa 31 zinazotarajiwa kushiriki kombe la FIFA la Dunia mwaka huu.

Marekani imewasili usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Doha ikiwa zimebaki siku 9 kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la FIFA la Dunia 2022.

Marekani imepangwa kundi B katika michuano ya mwaka huu pamoja na England, Wales na Iran

Michuano ya Kombe la FIFA la Dunia inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 20, 2022 na kufikia kilele Disemba 18, 2022.