Simba Queens Leo majira ya saa moja jioni watashuka katika dimba la Prince Moulay Al Hassan mjini Rabat nchini Morocco kuumana na Mamelod Sundown katika mchezo wa nusu fainali ya kihistoria kwa upande wa Simba inayowakilisha Klabu za soka za wanawake katika ukanda wa CECAFA.
Simba Queens wamefikia hatua hiyo baada ya kuibuka washindi wa pili katika kundi A nyuma ya ASFAR Club ya Morocco.
Mamelod Sundown ladies ambao ni Mabingwa wa michuano hiyo waliibuka vinara wa kundi B na hivyo mchezo wa leo utakua na ushindani mkubwa.
Kocha wa Simba Queens Charles Lukula amewaambia waandishi wa habari mjini Rabat kuwa timu yake imekwenda kushindana na hivyo wapinzani wao wajiandae na ushindani kutoka kwao.