Spika Tulia akutana na Spika wa Gauteng

0
185

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amekutana na kufanya mazungumzo na
Spika wa Bunge la jimbo la Gauteng nchini Afrika Kusini ambaye pia ni mweka hazina wa chama cha Mabunge cha Jumuiya ya Madola (CPA)
Kanda ya Afrika Ntombi Mekgwe, alipomtembelea ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma leo Novemba 8, 2022.