Clatous Chama wa Simba na Stephen Aziz Ki wa Yanga wamefungiwa mechi tatu (3) na faini ya shilingi laki tano kila mmoja kwa kosa la kutosalimiana na wachezaji wa timu pinzani kwenye derby ya Kariakoo.
Taarifa ya TFF imeeleza kuwa wawili hao wamefungiwa kutokana na kitendo chao cha kukacha kusalimiana na wachezaji wenzao wakati wa mchezo baina ya miamba hiyo ya soka hapa nchini uliopigwa Oktoba 23 mwaka huu.
Taarifa ya TFF imeeleza kuwa kitendo hicho ni kinyume na kanuni ya 41:4(5.4) ya Ligi kuu kuhusu udhibiti wa wachezaji.
TFF pia imeitoza faini ya shilingi milioni 5 klabu ya soka ya Yanga kwa kosa la kuingilia mlango usioruhusiwa wakati wa mchezo baina yake na Simba uliopigwa Oktoba 23 mwaka huu katika dimba la Benjamin Mkapa mkoani Dar es Salaam.
Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 17:(22 na 60) ya Ligi kuu kuhusu taratibu za mchezo.