Aliyetoa penati tata Geita vs Yanga kikaangoni

0
161

Mwamuzi Florentina Zabron aliyesimama kati kwenye mchezo wa Geita dhidi ya Yanga amepelekwa kwenye kamati ya Waamuzi ambao watarejea tukio lake la penati ya utata kisha wataishauri kamati ya nidhamu ya TFF

Taarifa ya TFF imeeleza kuwa baada ya Kamati ya waamuzi kulipitia kitaalam tukio hilo itaishauri TFF hatua za kuchukua dhidi ya Mwamuzi huyo.

Mechi hiyo iliyochezwa katika dimba la CCM Kirumba Oktoba 29 mwaka huu, ilimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1 kwa bila.