Ajali yaua watu saba Kiteto

0
149

Watu saba wamefariki dunia na wengine wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea kwenye eneo la pori namba moja wilayani Kiteto mkoani Manyara.

Habari zinaeleza kuwa ajali hiyo imehusisha gari la kubeba wagonjwa ambalo limegongana uso kwa uso na gari nyingine aina ya Prado.

Majeruhi watano wa ajali hiyo wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma na wengine katika hospitali ya wilaya ya Kiteto.

Habari zaidi zinaeleza kuwa gari la kubeba wagonjwa lililopata ajali ni la kituo cha afya cha Sunya wilayani Kiteto na lilikuwa linatoka Kibaya kupeleka mgonjwa na baada ya kushusha mgonjwa lilikuwa likirejea kwenye kituo chake cha Sunya.

Watu wote waliofariki dunia katika ajali hiyo walikuwa ndani ya gari hilo la kubeba wagonjwa.