Aliyeokoa manusura kuingizwa Jeshi la Zimamoto

0
277

Serikali imesema
kijana Majaliwa Jackson aliyesaidia kuwaokoa watu 26 katika ajali ya ndege mkoani Kagera, atapatiwa mafunzo ya uokoaji na kuingizwa ndani ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hilo ni agizo la Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ametaka Jackson apatiwe mafunzo hayo na aingizwe katika Jeshi hilo la Zimamoto na Uokoaji.

Waziri Mkuu Majaliwa amemkadhi kijana huyo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni ili aweze kuteleleze agizo hilo la Rais Samia Suluhu Hassan.

Waziri Mkuu ameyasema hayo katika uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera,, alipoongoza mamia ya waombolezaji katika kuaga miili ya watu 19 waliofariki dunia katika ajali hiyo ya ndege iliyotokea kwenye ziwa Victoria.

Pia amesema, Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza mazishi ya watu wote 19 waliofariki dunia katika ajali hiyo yagharamiwe na serikali.