Rais atoa pole ajali ya ndege Kagera

0
310

Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa wafiwa wote na majeruhi wa ajali ya ndege iliyotokea hapo jana Bukoba mkoani Kagera na kusababisha vifo vya watu 19.

Rais Samia pia amewashukuru wakazi wa Kagera kwa ujasiri, ushirikiano na jitihada walizofanya kuwaokoa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo ambayo ni mali ya Shirika la Ndege la Precision.