Pole Tanzania

0
119

Tunatoa salamu za pole kwa waathirika wote pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wa watu 19 waliofariki dunia katika ajali ya ndege iliyotokea Bukoba mkoani Kagera Novemba 06, 2022.

Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu uponyaji wa haraka majeruhi wote, na kwa marehemu tunawaombea wapumzike kwa amani.