Waziri Mkuu: Kazi ya Kuwaokoa watu imekamilika

0
288

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasili Mjini Bukoba mkoani Kagera, kuangalia zoezi la uokoaji kufuatiia ajali ya ndege ya Shirika la ndege la Precision iliyotokea mapema hii leo.

Akizungumza na wakazi wa Bukoba Waziri Mkuu amesema kazi ya kuwaokoa watu wote kwenye ndege imekamilika na kitakachofanyika hivi sasa ni kuondoa mizigo ya watu waliokuwamo ndani.

Tayari watu 19 wamethibitika kufariki dunia mpaka sasa katika ajali hiyo iliyotokea wakati ndege hiyo ikiwa katika safari zake za kawaida kutoka Dar es Salaam kuelekea Bukoba.

uokoaji kufuatiia ajali ya ndege ya Shirika la ndege la Precision iliyotokea mapema hii leo.

Akizungumza na wakazi wa Bukoba Waziri Mkuu amesema kazi ya kuwaokoa watu wote kwenye ndege imekamilika na kitakachofanyika hivi sasa ni kuondoa mizigo ya watu waliokuwamo ndani.

Tayari watu 19 wamethibitika kufariki dunia mpaka sasa katika ajali hiyo iliyotokea wakati ndege hiyo ikiwa katika safari zake za kawaida kutoka Dar es Salaam kuelekea Bukoba.

Picha na Millard Ayo