Waliofariki ajali ya ndege wafikia 19

0
314

Watu 19 wamethibitika kufariki dunia katika ajali ya ndege inayomilikiwa na Shirika la Ndege la Precision, iliyotokea mapema hii leo mkoani Kagera.

Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Dar es kwenda Bukoba mkoani Kagera, na ilipata ajali hiyo ikiwa na watu 43 ndani.

Ajali hiyo imetokea katika ziwa Victoria, takribani mita 100 kabla ya ndege hiyo kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba.