Mtanzania ashinda tuzo Nigeria

0
190

Mtanzania Elizabeth Ayo, ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Mrembo Safaris, ni miongoni mwa wanawake waliotunukiwa tuzo katika tuzo za wanawake 100 waliofanya vizuri katika sekta mbalimbali Barani Afrika (AFRICA TRAVEL 100 WOMEN).

Tuzo hizo zilizotolewa huko Lagos, Nigeria zinatolewa kwa wanawake waliofanya vizuri zaidi katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na utalii, uongozi, utoaji huduma, anga, uhifadhi na habari.

Washiriki kutoka nchi 20 barani Afrika walikuwa wakiwania tuzo hizo zinazotolewa na taasisi ya AKWAABA Travel.