Mratibu wa Kituo cha Watu na Utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Profesa Herbert Qambalo amesema, matokeo ya sensa ya watu na makazi yatachochea maendeleo ya Taifa na wananchi kwa ujumla.
Profesa Qambalo ameyasema hayo katika mahojiano kwenye kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC 1.
Ameongeza kuwa matokeo hayo yatasaidia mipango ya serikali kulingana na idadi ya watu na kulingana na makundi yao kama vile wazee, wanawake, vijana na watoto.
Profesa Qambalo ametolea mfano idadi ya vijana ambapo amesema, serikali itatumia matokeo hayo kufanya maboresho katika mambo mbalimbali yanayowahusu.
Matokeo ya awali ya sensa ya watu na makazi kwa mwaka 2022, yanaonesha Tanzania ina watu 61.7.