Bunge lapitisha Muswada wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi

0
349
Kikao cha kwanza cha Mkutano wa Tisa wa Bunge la 12.

Bunge la Tanzania limepitisha Muswada wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi mwaka 2022, hivyo sasa unasubiri saini ya Rais kuweza kuwa sheria kamili.

Lengo la sheria hiyo ni kuweka masharti kuhusu misingi ya ulinzi wa taarifa binafsi kwa lengo la kuweka kiwango cha chini cha matakwa ya ukusanyaji na uchakataji wa taarifa binafsi, kuanzisha Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, kuimarisha ulinzi wa taarifa binafsi zinazochakatwa na vyombo vya Serikali na vyombo binafsi, na masuala mengine yanayohusiana na hayo.

Katika hatua nyingine Bunge limepitisha Muswada wa Sheria ya Uwekezaji Tanzania mwaka 2022 ambao unalenga kuweka masharti ya uwekezaji Tanzania, kuweka masharti ya mazingira bora kwa wawekezaji, kuweka mfumo wa kitaasisi kwa ajili ya uratibu na uwezeshaji wa uwekezaji nchini, kufuta Sheria ya Uwekezaji Tanzania, 1997 na masuala yanayohusiana na hayo.