Nishati safi ya kupikia kutengewa bajeti

0
263

Akizungumza mkoani Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Mjadala wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia, Rais Samia Suluhu Hassan amesema katika mwaka ujao wa fedha, nishati safi ya kupikia itatengewa fungu lake.

“Nimetoa pendekezo la kuunda kikosi kazi cha kuangalia kuhusu kuhamia kwenye nishati safi ya kupikia. Bajeti ijayo tutakwenda kutenga fedha ya kutosha kwa ajili ya mfuko wa nishati safi ya kupikia.” amesema Rais Samia

Aidha, ameitaka mikoa inayoongoza kwa ukataji holela wa misitu; Pwani, Morogoro, Tabora, Lindi na Ruvuma kupunguza kufanya hivyo ili kulinda mazingira.