Dkt. Chana aweka kambi mlima Kilimanjaro

0
284

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Pindi Chana ameweka kambi katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro, ili kuhakikisha moto unaowaka kwenye maeneo machache yaliyosalia ya mlima huo unazimwa.

Akiwa katika hifadhi hiyo, Dkt. Chana amepokea taarifa ya utekelezaji wa kazi inayoendelea ya kuzima moto huku akiwashukuru na kuwapongeza wadau wote waliojitolea kuhakikisha moto unadhibitiwa katika maeneo yote.

Ameendelea kukemea tabia ya baadhi ya wananchi wanaoanzisha au kuchoma moto hovyo katika maeneo yaliyohifadhiwa na kuisababishia Serikali na wananchi hasara kubwa.

Waziri huyo wa Maliasili na Utwlii amesisitiza kuwa, yeyote atakayebainika
kuchoma moto hovyo katika maeneo yaliyohifadhiwa atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

“Huu ni msimu wa maandalizi ya kilimo, natoa rai kwa ndugu zangu wakulima mnaopakana na Hifadhi za Taifa muwe makini pindi mnaposafisha mashamba yenu, msitumie moto bali tafuteni njia mbadala ili kuepusha moto, kuchoma misitu na kusababisha hasara kubwa, yeyote atakayesababisha moto kwenye Hifadhi za Taifa atachukuliwa hatua kali za kisheria.” amesisitiza Dkt. Chana