Uwanja wa Ndege Msalato kukamilika Desemba 2024

0
338

Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato mkoani Dodoma unatarajiwa kukanmilila Desemba 2024, ikiwa ni miezi 36 tangu ujenzi wake ulipoanza Aprili 2022 na Septemba 2022 kwa sehemu ya kwanza na ya pili ya awamu ya kwanza ya ujenzi.

Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala la Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Rogatus Mativila, wakati akitoa taarifa ya mradi huo unaojengwa kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambayo imetoa dola milioni 329 za Kimarekani.

Katika awamu ya kwanza ya ujenzi, uwanja huo utakuwa na hadhi ya daraja 4E, na utaweza kupokea ndege kubwa kama Boeing Dreamliner 787, na upanuzi utaendelea kufanyika kutoka kuhudumia watu milioni 1.5 kwa mwaka hadi zaidi ya watu milioni 30 baada miaka 100.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika nchini, Patricia Laverley amesema uwanja huo utatimiza azma ya Serikali ya kuhamia Dodoma, kwa ndege kubwa kuweza kufanya safari za moja kwa kutoka Dodoma kwenda sehemu yoyote duniani.