Mtanzania atwaa taji la Miss Kiziwi Dunia

0
280

Mrembo wa Tanzania Hadija Kanyama ametwaa taji la urembo la dunia kwa viziwi kwa upande wa wanawake (Miss Deaf World 2022), katika mashindano ya Dunia ya Urembo, Utanashati na Mitindo kwa Viziwi Duniani.Mashindano hayo yamefanyika usiku wa kuamkia hii leo katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere mkoani Dar es Salaam (JNICC), ambapo Hadija amewashinda warembo wengine 12.

Mbali na kuwa Miss Kiziwi Dunia kwa mwaka 2022, Hadija pia ameshinda kipengelle cha Miss kwenye kucheza muziki wa asili.

Kwa upande wa wanaume, Gareth Kelaat kutoka Australia ndiye ametangazwa Mr. Kiziwi Dunia kwa mwaka 2022 baada ya kuwabwaga wenzake saba kutoka mataifa mbalimbali.

Washindi hao wamepatikana kufuatia uamuzi wa jopo la majaji nane wakiongozwa na Rais wamashindano hayo ya Dunia ya Urembo, Utanashati na Mitindo kwa Viziwi Duniani kutoka nchini Marekani, Baneta Ann Li.

Tanzania imekuwa nchi ya kwanza katika Bara la Afrika na ya 12 duniani kuwa mwenyeji mashindano hayo ya Dunia ya Urembo, Utanashati na Mitindo kwa Viziwi Duniani.