Maandalizi kwa ajili ya uzinduzi wa matokeo ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika Agosti 23 mwaka huu yamekamilika.
Kamisaa wa sensa ya watu na makazi 2022 kwa upande wa Zanzibar Balozi Mohamed Haji Hamza, ameyasema hayo wakati wa mahojiano na TBC1 katika kipindi cha Jambo Tanzania.
“Sisi wataalamu na wasimamizi tunasema kwamba shughuli hizi zimekwenda vizuri, tumeshachakata matokeo na matokeo sasa yapo tayari.” amesema Balozi Mohamed Haji Hamza
https://www.youtube.com/watch?v=3AGfRMIdovA
Ameongeza kuwa ukiachana na uzinduzi wa matokeo ya sensa ya watu na makazi, pia kutazinduliwa mwongozo wa matumizi ya taarifa zitakazotokana na takwimu za sensa ya watu na makazi ambapo mgeni anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassa
“Tupo kwenye maandalizi na tunategemea tarehe 31/10/2022 Rais Samia Suluhu Hassan kuzindua matokeo haya katika uwanja wa Jamhuri hapa mjini Dodoma.” amesema Balozi Mohamed Haji Hamza