Watuhumiwa 1212 wa dawa za kulevya mbaroni

0
373

Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na dawa za kulevya Amon Kakwale amesema, watuhumiwa 1212 wa dawa za kulevya wamekamatwa katika operesheni iliyofanyika nchi nzima.

Amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika operesheni iliyoendeshwa nchi nzima kuanzia Septemba Mosi mwaka huu hadi tarehe 25 mwezi huu.

Kakwale amesema
operesheni hiyo imeshirikisha Jeshi la Polisi nchini kupitia kitengo hicho cha Kuzuia na Kupambana na dawa za kulevya na Polisi wa mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa lengo la kukabiliana na uhalifu na wahalifu wa dawa za kulevya.

Amesema dawa za kulevya zilizokamatwa kwa kipindi hicho ni bangi kilo 1962.154, mirungi kilo 1081.73, Heroin gramu 448.74 pamoja na kuteketeza mashamba ya bangi hekari 9.55 na miche ya mirungi 220.