Mtu mchafu zaidi duniani afariki dunia

0
325

Amou Haji, raia wa Iran aliyepewa jina la utani la mtu mchafu zaidi duniani kwa sababu za kukataa kuoga kwa zaidi ya miaka hamsini amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 94.

Shirika la habari la Iran limeeleza kuwa Amou amefariki dunia katika kijiji cha Dejgah kilichopo kwenye jimbo la Fars, huku sababu za kifo chake zikitajwa ni uzee.

Mara kadhaa mtu huyo ambaye ni mwanamume alisikika akisema hataki kuoga akiamini akifanya hivyo atafatiki dunia, na alikwepa majaribio kadhaa ya wanakijiji wenzake waliotaka kumuogesha kwa lazima.

Mwaka 2014, gazeti la Tehran Times liliripoti kuwa mtu huyo alikuwa akivuta au kunusa bomba lililojaa kinyesi cha mnyama na aliamini kuwa msafi kungemfanya awe mgonjwa.