WhatsApp ‘Down’

0
305

Watumiaji wa mtandao wa WhatsApp duniani kote wamejikuta wakituma jumbe mbalimbali bila mafanikio kutokana na hitilafu kwenye mtandao huo unaomilikiwa na kampuni ya Meta.

“Tunafahamu kuwa baadhi ya watu kwa sasa wanashindwa kutuma ujumbe na tunajitahidi kurejesha WhatsApp kwa kila mtu haraka iwezekanavyo,” umesema uongozi wa kampuni hiyo ya Meta.

Kufuatia hitilafu hiyo, watumiaji wa mtandao huo wa Whatsapp wamelazimika kuhama na kwenda kutumia mitandao mingine.